Mkurugenzi wa Wasafibet Nasibu Abdul amezindua Promosheni mpya ya Jipate na EURO katika kipindi hiki cha michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Juni 14 nchini Ujerumani.
Akizungumza na Waandishi wa habari makao makuu ya ofisi za Wasafibet jijini Dar es Salaam, Nassib amesema kuwa ndani ya Msimu wa michuano ya EURO kuna watanzania wataondoka na zawadi nono.
“Cheza EURO ndani ya App ya #Wasafibet uondoke na Zawadi kemkem kutoka kwetu”, amesema Nassib.
Ameongeza kuwa kampeni hiyo ni kwa wateja wapya na wazamani, huku vigezo na masharti kuzingatiwa katika kupata washindi.
Awali Wasafibet ilikabidhi hundi ya shilingi milioni ishirini (20,0000,000/-) kwa mshindi wa kampeni ya maokoto ya EPL 2023/2024 Saidi Daudi kutoka mkoani Tabora.