Kampuni ya Mawasiliano, Tigo imezindua rasmi Sako kwa Bako na Energizer ambapo wamekuja na simujanja mpya ya Energizer U652S.

Simu hiyo ya Energizer U652S itapatikana kwa bei ya TZS 199,000 na itauzwa kwenye maduka yote ya Tigo pekee nchini nzima.

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi huo,Afisa Mkuu wa Biashara kutoka Tigo Isack Nchunda alisema uzinduzi huo ni mwendelezo wa kampeni  iliyopata mwitikio mzuri kutoka kwa wateja wao ya 'Sako Kwa Bako,' ambayo imelenga kuimarisha mahusiano yao na wateja wake na kusherehekea hatua kubwa ya kufikia zaidi ya wateja milioni 20. 

Nchunda alisema simu hiyo mpya imetengenezwa kukidhi mahitaji ya wateja wao huku ikiwa imesheheni sifa lukuki.

Alisema wateja wanaonunua Energizer U652S watapata kifurushi cha intaneti cha GB78 BURE kwa mwaka mzima ambapo  Ili kupata ofa hiyo wateja watahitaji kuweka vocha ya TZS 2,000 kila mwezi kwa ajili ya kupokea kifurushi hicho. 

"Hii ni ofa adhimu kuwezesha wateja wetu kufurahia intaneti yetu ya 4G iliyoenea nzhi nzima.  

Energizer U652S ni toleo jipya zaidi katika orodha yetu ya simujanja zenye sifa bora, kuhakikisha wateja wetu wanafurahia teknolojia ya kisasa"

"Simujanja ya Energizer U652S ni mfano wa namna bora ya kufikia lengo hili ambapo pia simu hii inapatikana kwa bei rafiki/nafuu kwa wateja wetu wote. Kwa kufanya hivi, sio tu tunachangia watanzania kufikiwa na huduma za kidigitali kwa wingi zaidi bali pia tunahakikisha wanapata uzoefu mzuri wa kidigitali."

Nchunda amewaahidi wateja wake kuendelea kutoa huduma bora ambazo zinakidhi mahitaji yao.

"Hii ni ishara ya imani na uaminifu mkubwa ambao wateja wetu wameweka kwetu, na tunaahidi kuendelea kutoa huduma na bidhaa bora zinazokidhi mahitaji yao."

 Wakati wa uzinduzi wa kampeni ya 'Sako Kwa Bako' Kampuni ya Tigo waliahidi kwamba watatoa bidhaa na huduma 2 / 2

zinazogusa maisha ya wateja wetu, hivyo Jana  tunatimiza ahadi hiyo kwa kuzindua simujanja hiyo.

Kwa upande wake , Mkuu wa Kitengo Cha ukuzaji wa masoko, Daniel Nnko aliwakaribisha wateja wote kwenda kutembelea katika maduka yote ya Tigo ili kujipatia simu hiyo iliyoambatana na ofa.

Share with Others