Na Lilian Ekonga, Dar es salaam.
Wamiliki wa nembo nchini wametakiwa kuhakikisha wanafuatilia bidhaa zao sokoni na kutoa taarifa katika Tume ya ushindani (FCC) pale wanapo baini uwepo wa bidhaa zinazoiga alama za bidhaa zao kwa maana ya bidhaa bandia.
Ameyasema hayo leo Julai 18 ,Naibu Waziri Wizara ya Viwanda na Bishara, Mhe Exaud Kigahe wakati akimwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika Kongamano la maadhimisho ya kuthibiti bidhaa bandia Duniani.
"Wamiliki wanapaswa kutoa elimu kwa umma kuhusiana na bidhaa Zao na hii elimu itawasaidia walaji kutofautisha bidhaa halisi na zile bidhaa feki na kusaidia walaji kununua bidhaa halisi" amesema Kigahe
Ameongeza kuwa wakala wa ushuru wa forodha kuhakikusha wanakuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanashirikiana na fcc katika kudhibiti bidhaa bandia kuto kuingia nchini.
Alikadhalika amewatak wadhalishaji na wafanyabishara nchini kuhakikisha wanapofanya biashara zao zinakidhi sheria ya alama za bidhaa ya mwaka 1993 inayosimamia udhibiti wa bidhaa bandia.
"Sheria hii inakataza kuingiza, kutengeneza, kuuza na kuhifadhi bidhaa bandia ambapo adhabu yake ni kifungo au kulipa faini kama ambavyo imelezwa kwenye sheria hii"amesema
Aidha ameiomba Fcc kushirikiana na wamiliki wa nembo na mamlaka nyingine za serikali katika kuimarisha udhibiti wa biashara haramu za bidhaa bandia na kuhakikisha kuwa wawekezaji wanakuwa na imani ya kuwekeza nchini.
"Udhibiti wa bidhaa bandia si wajimu wa mtu mmoja bali zinagitajika juhudi za pamoja katika kuhakikisha kuwa tunalinda masoko yetu na hivyo kuvutia wawekezaji ambao watakuwa na imani bidhaa zao zinazozalishwa ndizo zinakuwa sokoni.
"Kwa kushirikiana na Fcc na wadau wengine tutahakikisha udhibiti wa bidhaa bandia unakuwa na mafanikio zaidi hasa katika maeneo ya ushirikiano wa kupata mafunzo na nyenzo za kisasa za kutambua na kuthibiti bidhaa bandia"
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya ushindani FCC William Erio alisema kuwa licha ya elimu kutolewa kwa wananchi juu ya utambuzi wa bidhaa bandia bado kuna haja ya kuendelea kuzungumza na wafanyabiashara umuhimu wa kuweka alama au nembo katika bidhaa zao huku Ummy Mohamed Rajab kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa ZFCC amesema athari za matumizi ya bidhaa bandia hazilengi kudumaza uchumi wa nchi pekee bali hata kwa watumiaji.
Aidha alizitaja shughuli mbalimbali zilizofanyika tangu kuanza kwa maadhimisho hayo hadi kilele chake ambazo ni pamoja na utoaji elimu wa kuacha matumizi ya bidhaa bandia kupitia vyombo vya habari, kufanya moanesho ya wamiliki bidhaa katika ukumbi wa mlimani city Jijini Dar es salaam.
Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu Kanda ya Dar es salaam, salma Maghimbi amesema mahakama itaendelea kutimizia jukumu muhimu katika kutafsiri sheria na kanuni na kuhakikisha kwamba wahalifu wa bidhaa bandia wanawajibishwa ipasavyo mbele ya sheria.