WAZIRI wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ajira Vijana na wenye ulemavu, Deogratias Ndejembi amesema serikali ya awamu ya sita tangu ilipoingia madarakani, imeweka mazingira rafiki ya uwekezaji ambayo inakuza ajira na fursa mbalimbali ambazo watanzania wanaweza kuzitumia.

Ndejembi ametoa wito huo Julai 7,2024 wakati alipotembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu linalojumuisha taasisi zote zilizopo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu iliyo chini ya Wizara mbili Kazi, vijana, ajira na watu wenye ulemavu pamoja na Sera,bunge na uratibu.

Amewataka wananchi kuendelea kutembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu ili kujionea shughuli mbalimbali za uratibu zinazofanyika na fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali ya awamu ya sita ,inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema katika banda hilo kuna taasisi zinazoratibu shughuli mbalimbali ikiwemo kuwezesha wananchi kiuchumi makundi mbalimbali ikiwemo vijana, wanawake, wenye ulemavu na kuonesha fursa zilizopo na zinazotolewa na Serikali ya awamu ya Sita,inayoongozwa na Rais Dkt. Samia.

Amesema banda hilo linaonesha dhana nzima ya uratibu unaofanyika ndani ya serikali ya ofisi ya Waziri Mkuu.

Amesema kwenye maonesho hayo huduma zote zinazoratibiwa na serikali zinapatikana ikiwemo fursa za vijana.

Amesema kwa siku ya Julai 5, pekee, wananchi waliotembelea maoneaho hayo walikuwa zaidi ya 52,000.

“Wingi huu wa wananchi inaonesha nanmna gani nchi imefunguka kutokana na uongozi mahiri wa Rais Samia na inaonesha namna gani wafanyabiashara walivyoikimbilia Tanzania kuwekeza,”amesema.

Share with Others