Mkuu wa Mkoa wa Dares Salaam, Albert Chalamila amesema mpaka Jana jumla ya watu waliofariki dunia kutokana na kuporomoka kwa jengo la ghorofa Kariakoo ilikuwa ni wanne huku sababu ikiwa sio kukosa hewa.

Chalamila ameyasema hayo leo Jumapili Novemba 17, 2024 wakati shughuli za uokozi zikiendelea katika jengo hilo lililoporomoka jana Jumamosi Novemba16, 2024.

"Mpaka mudu huu waliokufa kwa safocation (kukosa hewa) hatuna taarifa hiyo na hii ni kwa taarifa ya papo kwa hapo," amesema Chalamila.

Amebainisha kuwa kwa wachache waliofariki dunia sababu ni kudondokewa na jengo, kuangukiaa na jiwe au kuchomwa na nondo.

Pia, amesema wanaendelea kuwasiliana na watu waliokwama chini ya jengo hilo na wamepelekewa gesi, maji na glucose huku wakiwaomba kuendelea kuwa wastahimilivu.

Share with Others