Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi nwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Simiyu Dk. Yahya Nawanda na kufanya uteuzi wa viongozi kadhaa.
Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu, imeeleza kuwa Rais Dkt. Samia amemteua Kenan Laban Kihongosi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
Kabla ya uteuzi, Kihongosi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba ambapo Kihongosi anachukua nafasi ya Dkt. Yahaya Ismail Nawanda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Rais pia amemteua Elias Daniel Mwandobo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba. Kabla ya uteuzi, Mwandobo alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais - Ikulu.
Amemteua Christopher Magala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Magala anachukua nafasi ya Dkt. Stephen Isaac Mwakajumilo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Amemteua George Hillary Herbert kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi, Bw. Herbert alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani.
Taarifa imeeleza kuwa, Uapisho wa Mkuu wa Mkoa na Msajili wa Mahakama ya Rufani utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.