Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema amedai vurugu zilizojitokeza juzi wakati wa uchaguzi wa viongozi wa Mkoa wa Arusha, zilipangwa kwa lengo la kuharibu uchaguzi huo.
Ameagiza viongozi wa mikoa na wilaya wanakotoka waliosababisha vurugu hizo, kuwasiliana na matawi wanayotoka na kuwavua uanachama kwa madai kuwa wamekidhalilisha chama hicho.
Lema ameyasema hayo leo Juammosi Novemba 16, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni siku chache tangu itokee sintofahamu, baada baadhi ya wanachama wa chama hicho kuleta vurugu wakituhumu uchaguzi huo kugubikwa na rushwa.
"Sasa ukiniuliza mimi kwamba ile fujo chanzo chake ni nini? Naibu Katibu Mkuu bara CHADEMA (Benson Kigaila) anaweza akawa na majibu ya hili, maneno haya isivyo bahati ninayasema, ila ninayasema kwa ajili ya kutunza uaminifu wangu, kwasababu nyinyi wanahabari hamkurekodi lile jambo kwenye vikao vya chama, haya nitayasema hadharani" Lema.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kaskazini Godbless Lema akizungumza na wanahabari mkoani Arusha Novemba 16, 2024 juu ya ugomvi wa wanachama wa chama hicho uliotokea hivi karibuni mkoani humo.