WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Deogratius Ndejembi, amesema utoaji huduma kupitia mtandao sio tu unaongeza ufanisi lakini pia unaongeza uwazi zadi.

Ndejembi ameyasema hayo baada ya kupatiwa maelezo ya huduma ya PSSSF Kidigitali, ambapo mwanachama kupitia Application ya PSSSF Kiganjani Mobile App, anaweza kupata taarifa zote zinazohusiana na uanachama wake katika Mfuko, wakati alipotembeela banda la PSSSF kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam kwenye viwanja vya Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam Julai 7, 2024.

“Matumizi ya Tehama inamuwezesha mwanachama kuona michango yake tangu alipoajiriwa, anaona amechangia kiasi gani, mwajiri wake ameleta kiasi gani, matumzii haya yanaleta uwazi mkuwba sana kwa jamii nzima inayocvhangia kwenye Mfuko.” Alifafanua.

Alisema, kustaafu si jambo la dharura, kila mtu anafahamu ifikapo miaka 55 kwa hiari na 60 kwa mujibu wa sharia, ni vema mtu akajiandaa mapema.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Abdul-Razak Badru amesema, Maonesho hayo yamewawezesha kuwahudumia wanachama wa Mfuko ambao wameweza kuoa michango yao, lakini pia kupata elimu ya matumizi ya PSSSF Kiganjani.

“Baadhi ya wanachama wanakwenda katika baadhi ya shughuli ambazo mMfuko umekwua ukifanya kwenye maonesho hayo.” Alifafanua.

Naye Mkurugenzi wa Uendeshaji PSSSF, Mbaruku Magawa ametoa wito kwa wanachama kutumia simu janza kupata huduma zinazohusiana na uanachama wao kwa njia rahisi.

Share with Others