Serikali kupitia Wizara ya Maji imeingia makubaliano ya ushirikiano na Kampuni ya Shanxi ya Utafiti wa Madini juu ya kufanya utafiti wa kihaidrojia katika rasilimali maji chini ya ardhi utakaofanyika katika vijiji takribani 10 katika Mkoa wa Dodoma.
Makubaliano hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Andrew Kundo (Mb), na Naibu Katibu Mkuu Ndugu Agness Meena pamoja na viongozi waandamizi Wizara ya Maji.
Utafiti huu unalenga kutoa suluhu ya upatikanaji wa maji katika maeneo ya mji wa Dodoma kupitia rasilimali maji ya chini ya Ardhi.
Hafla ya utiaji saini imekuwa ni sehemu ya maadhimisho ya kusherekea mahusiano ya kidiplomasia ya miaka 60 kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama Cha Kijamaa cha China (CCP) ikiwa ni ishara ya kuboresha na kudumisha mahusiano ya kimaendeleo baina ya nchi hizi mbili Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na China.