Historia ya gwiji huyu ilianzia siku alipozaliw,a tarehe 23 Machi mwaka 1955, katika eneo la Kariakoo. Mama yake alikuwa mama wa nyumbani wakati baba yake alikuwa anafanya shughuli za uchapishaji.
Maisha yake ya utoto yalikuwa ya kawaida ila alikuwa akipenda sana uimbaji wa Tabu Ley na mwimbaji mmoja wa Guinea Sorry Kandia. Alisoma shule ya Msingi ikiambatana na elimu ya Madrasa. Mwaka 1970 Akiwa bado shuleni, utaona umri wake ulikuwa miaka 15 tu, alijiunga na STC Jazz, ikiwa chini ya mpiga gitaa maarufu wakati huo Raphael Sabuni, kabla ya hapo bendi hii ilikuwa ikijulikana kama The Jets.