Mwigizaji wa Bongo Movie
Fredy Kiluswa amefariki dunia leo Novemba 16,2024 akipatiwa matibabu katika Hospital ya rufaa Mloganzila.
Taarifa hiyo imethibitishwa na
Mwigizaji mwenzie JB amethibitisha kufariki kwa mmoja wa Waigizaji ambao alikuwa akifanya nao kazi kwa karibu ambaye pia ni Mwigizaji wa filamu Nchini Fred Kiluswa aliyefariki Dunia wakati akipatiwa matibabu Hospitalini.
JB amesema kuwa "Ni kweli nimepigiwa simu amefariki, nilikuwa nina taarifa kwamba jana alikuwa Muhimbili a baadaye akapelekwa Mloganzila, presha ilikuwa haishuki na sasa hivi nimepigiwa amefariki, tulimchangia kwa ajili ya matibabu, alikuwa na tatizo la moyo na baadaye akawa anapata dawa na moyo wake ulikuwa unaenda vizuri lakini baadaye presha ikapanda akaanguka akapelekwa Muhimbili, presha haikushuka tena ndio amefariki, alikuwa anaumwa"
Marehemu Fredy Kiluswa alikuwa akicheza filamu tofauti tofauti na amewahi kufanya kazi na JB, Irene Uwoya na Mastaa Wengine.