Makamu wa Rais wa Malawi, Saulos Chilima, Amefariki Katika Ajali ya Ndege.

Taarifa rasmi kutoka Ofisi ya Rais nchini Malawi imetolewa, ikisema kuwa Makamu wa Rais wa Malawi, Saulos Klaus, amethibitishwa kufariki katika ajali ya ndege.

Ndege hiyo, iliyokuwa ikimbeba Makamu wa Rais, Dr. Saulos Klaus Chilima, na watu wengine tisa, ilipatikana asubuhi ya leo katika msitu wa Chikangawa, Malawi.

Abiria wote waliokuwemo ndani ya ndege hiyo wamefariki katika ajali hiyo.

Taarifa za Awali zilidai kuwa Ndege hiyo ya Jeshi la Ulinzi la Malawi "ilitoweka kwenye rada" baada ya kuondoka katika mji mkuu, Lilongwe, Jumatatu asubuhi.

Katika hotuba yake Jumatatu jioni, Rais Lazarus Chakwera alisema operesheni ya kuwasaka na kuwaokoa watu inaendelea.

Ndege hiyo ilitakiwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mzuzu, kaskazini mwa nchi hiyo, mara tu baada ya saa 10:00 kwa saa za huko (09:00 BST).

Share with Others