Lyiv, Ukraine. Mfululizo wa mashambulizi ya nguvu ya Russia dhidi ya miundombinu ya kijeshi huko Lviv, Ukraine, yamesababisha vifo vya watu kadhaa na mji wa magharibi mwa Ukraine kuwaka moto. Mji huo uliepushwa na mapigano makali hapo awali.

Mkazi wa Lviv aliliambia shirika la habari la AFP kwamba waliona moshi mwingi ukipanda juu ya majengo ya makazi na ving’ora vya mashambulizi ya anga vilisikika katika jiji lote wakati na baada ya shambulizi hilo.

“Kwa sasa, tunaweza kuthibitisha watu sita wamekufa na wanane wamejeruhiwa. Mtoto alikuwa miongoni mwa waathirika,” alisema gavana wa mkoa wa Lviv, Maksym Kozytsky kwenye mtandao wa kijamii.

Alisema makombora manne ya Russia yalilenga miundombinu ya kijeshi ya Ukraine na kituo cha matairi ya gari pia kilishambuliwa.

“Moto ulizimwa kutokana na mgomo huo. Bado unazimwa. Vifaa viliharibiwa vibaya,” alisema Kozytsky.

Andrei (21), mkazi wa Lviv alisema alikuwa amelala wakati ving’ora vikilia saa 2 asubuhi.

Share with Others