Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Jokate Mwegelo amesema lengo kubwa la kuwasili mkoani Iringa ni mpango mkakati wa kuinua kituo cha Ihemi kuwa chachu na fursa zaidi kwa vijana huku akiwataka vijana wanaoaminiwa na kupewa nafasi za uongozi ndani ya chama au serikali kufanya kazi kwa bidii na kwa ubunifu kwa manufaa ya Taifa.

 Jokate ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao na viongozi wa Chama na Jumuiya ya UVCCM Mkoa wa Iringa mara baada ya kuwasili na kupokea taarifa ya kazi ya UVCCM mkoani humo


"Tumekuja hapa kuangalia fursa za kuendeleza kituo chetu cha Ihemi na hivi karibuni tutakuwa na mafunzo kwa viongozi wetu wa wilaya nchi nzima." Jokate Mwegelo

Share with Others