Jogoo wa Soka Christiano Ronaldo ametangaza kufiwa na mtoto wake wa kiume aliyetarajiwa kuzaliwa.
Katika taarifa yake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter Ronaldo anayewika hivi sasa Manchester United, amesema yeye na mzazi mwenziye walikuwa wakitarajia kupata watoto mapacha wa kike na kiume, lakini kwa masikitiko wa kiume amefariki na wakike ametoka salama.
“Kwa masikitiko makubwa tunatangaza kuwa mtoto wetu wa kiume amefariki.Ni maumivu makubwa sana kwa mzazi yeyote kuyapata.Ni kuzaliwa salama kwa binti yetu ndiyo walau lina tupa matumaini na furaha” aliandika Ronaldo muda mfupi iliyopita.
Ronaldo na mwenza wake huyo Georgina Rodriguez wana mtoto wa kike Alana Martina aliyezaliwa 2017. Lakini ana watoto wengine Christiano Jr aliyezaliwa 2010 na mapacha Eva na Mateo.
Mchezaji mwenzake Marcus Rashford aliandika” Tuko pamoja nawe kaka.. pole sana”
Manchester United Jumanne hii 19th April watakuwa Anfield kucheza na Liverpool katika mechi za ligi kuu ya Uingereza na kwa msiba huo huenda United ikakosa huduma ya Ronaldo ambaye mwisho kwa wiki alipachika mabao 3 katika ushindi wa United wa mabao 3-2 dhidi ya Norwich.
Aboubakary Liongo
Moonlight Media