Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es salam na Pwani inaendelea kuimarika baada ya kukamilika kwa matengenezo yaliyotokana na hitilafu ya umeme iliyotokea wiki iliyopita katika mitambo ya Uzalishaji maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini mkaoni Pwani.
Huduma hiyo ya maji imeanza kurejea na inaendelea kupatikana vizuri katika maeneo tofauti yakiwemo Makongo, Ubungo, Kibo, Kimara, Tabata, Segerea na maeneo mengine ambayo sasa msukumo wa maji unaendelea kuongezeka na kuwafikia wateja mbalimbali.
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) ilitangaza kwa umma dharura ya kusimama kwa usambazaji wa huduma ya maji kwa wateja wanaohudumiwa vyanzo vya Ruvu Juu na Ruvu Chini ili kupisha matengenezo ya umeme katika maeneo hayo.