Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Ummy Nderiananga amepongeza juhudi za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Dodoma (DUWASA) za kumtuma mama ndoo kichwani.

Nderiananga ametoa pongezi hizo mara baada ya kutembeleza banda la DUWASA wakati wa maonesho ya kitaifa ya kilimo, mifugo na uvuvi ya Nane Nane 2024.

Amesema DUWASA imefanyakazi kubwa ya kuhakikisha huduma ya maji inawafikia wananchi wengi zaidi kwa kuiishi kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo kichwani.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Aron Joseph amesema mamlaka ikiwa ni mdau wa maendeleo katika sekta ya kilimo imeshiriki kwenye maonesho hayo kwa kuwa huduma ya maji haiwezi kutofautishwa na kilimo, mifugo na uvuvi.

Amesema DUWASA imetumia fursa ya maonesho hayo kuendeea kutoa elimu kwa wadau na kuonyesha vifaa vya teknolojia mbalimbali vinavyotumika kwa utafutaji wa maji ardhini, uzalishaji, usambazaji na huduma kwa wateja.

“Niwakaribishe wana Dodoma kufika kwenye banda letu kupata huduma huduma mbalimbali za maji na utahudumiwa vizuri zaidi,” amesema.

Share with Others