Afisa Usimamizi wa Mazingira wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Bi. Maria Holela leo Juni 04, 2024 ametoa Elimu ya Mazingira kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Viwandani.
Bi. Holela ametoa Elimu ya utunzaji wa mazingira ikiwemo vyanzo vya maji pamoja na matumizi sahihi ya mtandao wa majitaka ili kuepuka kuziba mara kwa mara ili kujiepusha na madhara.
Lengo la utoaji wa elimu hii kwa wanafunzi ni kuijenga jamii na kizazi kilichopo kutambua thamani na umuhimu wa utunzaji wa mazingira kwa huduma endelevu ya maji.
Maafisa wa Mazingira wa DUWASA wanaendelea na utoaji wa Elimu kwa Umma kuhusu dhana nzima ya utunzaji wa mazingira katika Maonesho ya Mazingira yanayoendelea katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Mjini Dodoma,ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani ambapo kilele chake ni Juni 05, 2024..