Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeibuka mshindi wa kwanza katika utoaji wa taarifa kwa umma miongoni Mwa Mamlaka za Maji Nchini.

Afisa Mawasiliano wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Ndugu Nelson Shoo akipokea tuzo kutoka kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye Waziri baada ya Mamlaka kuibuka kinara katika utoaji wa taarifa kwa umma miongoni Mwa Mamlaka za Maji Nchini, ameelekezwa kuwa tuzo hiyo ikawe chachu ya kufanya kazi zaidi.

Tuzo hiyo imetolewa na Waziri Nape wakati wa kikao kazi cha Maafisa Habari Serikalini kilichokuwa  na kauli mbiu. 

‘Jenga Mustakabali endelevu kwenye Sekta ya Habari katika zama za kidijiti’

Share with Others